ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Tuesday, July 31, 2018

July 31, 2018

Faida za Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Wakati wa Kufanya Mapenzi

Faida za Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Wakati wa Kufanya Mapenzi

jamiiforums.com

Aug 1, 2018 12:42 AM

1. Makalio makubwa husaidia kujua kama mwenzi wangu amefika orgasm, mfano ikitokeana hit Doggie basi wakati wa orgasm (most of girls) makalio huwayanatikisika (twitch, fasciculate ) ambayo huwa inaambatanana miguno ya kimhaba inayo fifia ambayo kabla ya hapo huwa ya sautikubwa... hii unifanya nijue what to do next kumzidishia utamu zaidi. Hii kitu inukuwa ngumu kunotice kwa msichana ambaye nimwembamba just have to relay from other signs

2. Makalio makubwa huwa yananifanifanya iwe rahisi kwangu kuyashika (grab) especially wakati wa doggie.ikizingatia gym imekubali na kifua na mabega yametanuka ( shoulder to shouler distance ni kubwa). itaniwia ngumu sana kama msichana an mwili mdogo na makalio yake pia

3. Msichana mwenye makalio makubwa obvious atakuwa na nyama nyama kwenye mapaja hii nyama nyama zinakuwa na act kama chock absober na kucushion ile hiting force ,especially when adrenaline na sympathetic flow is at peak and s3x is becoming hardcore, katika situation hiii , kimbau mbau anaweza teguka nyonga. if ur not doing that smoothly.

4. Makalio makubwa yana yanasaidia kutengeneza ile NUMBER 8 ya mwili, mfano ukutane na msichana makalio makubwa na ni mtu wa mazoezi hana na mikunjo ya kunenepa mgongoni na tumboni , and ur hitting doggie, ukitazama her PERFECT ARCH from the behind yaani ni full Hamasa.

Kwa kumalizia siwabagui na kuwanyanyapaa wasichana wembamba, kwani kwenye haya mambo siku zote ni combination ya vitu vingi. Wembamba nao wana vitu adimu.. Its just me from what i ahave been experiencing....

Unaweza kutoa na wewe uzoefu wako ama kukosoa nilichoandika

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

125Chukia

COPY SUCCESS

Monday, July 30, 2018

July 30, 2018

KCB BANK TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA

KCB BANK TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA
Erasto blog.com

Jul 30, 2018 11:23 AM

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario  na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia wakikabidhiana mkataba baada ya kusaini Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420.000.000  katika hoteli ya Serena leo jijini Dar es salaam kulia ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420.000.000 kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya kusaini  mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCM Bi. Fatma Chilo wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa KCB Bank na TFF.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario akizungumza katika mkutano huo.

Baadhi ya watendaji wa benki ya KCB wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio katika mkutano huo.

………………………………………………………………….

KCB Bank Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa mwaka 2018/2019. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania 420,000,000 ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
KCB Bank Tanzania imeongeza thamani ya udhamini wake kwenda ligi hiyo kutoka kiasi cha shilingi za Kitanzania 325,000,000 msimu wa 2017/18 mpaka shilingi 420,000,000 msimu wa 2018/19 ongezeko la ziadi ya milioni 90,000,000, ongezeko linaloashiria dhamira ya benki hiyo kutaka kunyanyua vipaji na kuendeleza ushindani katika mpira wa miguu nchini Tanzania.
Hafla ya kutia saini makubaliano hayo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi. Fatma Chillo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi KCB Bank Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba mchango wa kiuchumi unaoletwa na soka ni mmoja sababu kubwa zilizopelekea KCB Bank Tanzania kutaka kudhamini ligi hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo. “Tunaamini kuwa sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kwani ni chanzo cha ajira kwa watanzania hasa vijana.” alisema Nd. Kimario.
Kaimu Menyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi. Fatma Chillo alisema kuwa ni fursa ya kipekee kuweza kudhamini Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili. “Lengo letu ni kuleta hamasa kwa timu na mashabiki wa mpira wa miguu kwa kuzijengea timu, hata zile ndogo uwezo wa kifedha ili kuziwezesha kushindana kikamilifu hivyo kuongeza ushindani ndani ya ligi.” Alieleza Bi. Chillo.

Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru KCB Bank Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2018/19. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

155Chukia

COPY SUCCESS

July 30, 2018

magazeti ya tz leo july 31,2018

Leo July 31, Karibu kutazama kilichoandikwa katika Magazeti ya TANZANIA, Hard News, Udaku, Michezo

By
erasto nyika

on

July 31, 2018

COMMENTS

Good Morning Mtu wangu wa nguvu !! kutoka Tanzania leo July 31, 2018nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti lipo Gazeti, Mwananchi, Jamvi la Habari,Uhuru, Mtanzania, Tanzania Daima, Tanzanite, Mwanaspoti, Kiu na mengineyo.

LIVE MAGAZETI: Siri nje Jokate kuteuliwa, Mnyukano CCM asilia, Wahamiaji

RELATED ITEMSMAGAZETITZA HABARI

COMMENTS

← PREVIOUS STORYMadiwani wawili wa CHADEMA, mmoja wa CUF wafikishwa Mahakamani kwa rushwa

SOMA NA HIZI

Madiwani wawili wa CHADEMA, mmoja wa CUF wafikishwa Mahakamani kwa rushwa

“Ninapuuza upotoshaji uliofanyika kwenye kauli yangu” –Kheri James

Ishu ya kuhamia CCM, Kubenea katoa majibu

TUPIA COMMENTS

IDRIS: WEMA NINGEMLIPIA HATA MILIONI 100

MAMA KANUMBA: GABO AMENIGHARAMIA KUFIKA HAPA

HOME 

NIFAHAMU WASILIANA NAMI MATANGAZO MKITO PRIVACY POLICY TERMS AND CONDITIONS

Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi, kaa karibu na mimi kwa kubofya hapo chini ☟

Copyright © 2018, Haki Zote Zimehifadhiwa. | Content by erasto | Designe

July 30, 2018

Lavalava Azimia Jukwaani , ni Baada ya Kupigwa Busu na Shabiki.

Lavalava Azimia Jukwaani , ni Baada ya Kupigwa Busu na Shabiki.

ghafla.com

Jul 30, 2018 10:01 AM

Kuna video inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimunyesha msanii kutoka WCB, Lavalva akiwa jukwaani ana-perform na mara akapigwa busu na moja ya mashabiki zake wa kike aliyepanda jukwaani hapa na ghafla msanii huyo kudondoka na kuzimia.

Msanii huyo ambae baada ya kuzimia ilibidi kupatiwa huduma ya kwanza na kisha kusomewa dua na ndipo alipoamka  , haiafahamika kama swala hilo amelifanya kwa kiki au ilikuwa kweli alikuwa katika hali hiyo.

Hata hivyo hakuna kiongozi yoyote katika kundi hilo alielisemea hilo wala yeye mwenyewe kuhushu tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi na kuwafanya mashabiki waanze kuimba kwa nguvu kuwa msanii huyo amekufa.

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

182Chukia

COPY SUCCESS

July 30, 2018

Majibu ya Ukimwi ya Diamond Gumzo, Msururu wa Wanawake Wawekwa Mezani

Majibu ya Ukimwi ya Diamond Gumzo, Msururu wa Wanawake Wawekwa Mezani

udakuspecially.com

Jul 28, 2018 11:27 AM

DAR ES SALAAM: Baada ya mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuanika stika inyaoonesha amepima magonjwa yote, gumzo la aina yake limeibuka kwenye mitandao ya jamii huku kelele zaidi zikipigwa kwenye majibu hususan Ugonjwa wa Ukimwi.

Akiwa nchini Marekani katika ziara ya kimuziki hivi karibuni, Diamond aliweka ‘status’ kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram inayomuonesha mkononi amefunga stika maalum ya hospitali inayoashiria amefanyia vipimo vya mwili na ndipo mjadala mkali uliposhika kasi kama moto wa kifuu.

TUICHAMBUE KWANZA STATUS

Kwenye status hiyo ambayo hukaa muda mfupi na kuondoka, stika aliyoivaa mkononi ilionesha jina lake (Nasibu Abdul), tarehe aliyozaliwa (Oktoba 2, 1988) aliyofanya vipimo hivyo yaani Julai 22, mwaka huu huku akiambatanisha na ujumbe wa maandishi kwa lugha ya Kingereza.

Kwa tafsiri isiyo rasmi sana, ujumbe huo uliashiria kwamba; “ni vigumu kupima na kuhakikisha anarudi nyumbani bila maambukizi kwa kupima mwili mzima (full body checkup),” mwisho wa kunukuu.

BALAA LAANZIA HAPO

Mara baada ya kuandika ujumbe huo ulioonesha kwamba amechekiwa mwili mzima, wachangiaji mbalimbali waliochangia mtandaoni humo, walianza kujiongeza kwa kujadili suala zima la matokeo ya vipimo hivyo na zaidi kwao haikuwa katika majibu kama ya Homa ya Ini, Malaria au Kifua Kikuu bali wengi walijikita kwenye Ukimwi kwenye eneo hilo.Wapo walionesha wasiwasi na kupinga kuwa haiwezekani akawa salama lakini wapo pia ambao walisema inawezekana.

MREMBO ASHADADIA ISHU

Baada ya Diamond kuweka status hiyo, mrembo aliyejitaja kwa jina la Kei, aliinasa picha pamoja na ujumbe wake huo na kuiweka fasta kwenye akaunti yake ya Instagram huku akiiambatanishia maneno yake kama ifuatavyo:

“Kama Mond kapima ngoma.. basi Ukimwi haupo..ngoja na mimi nikapime kesho…”Maneno hayo yaliamsha uchangiaji wenye mgongano wa hoja kwa baadhi ya marafiki wa msichana huyo ambapo wengi walimshambulia kwa kujaribu kutilia shaka vipimo vya afya alivyofanya Diamond huko Marekani.

“Mshamba tu wewe, kupima kwake kunakuhusu nini au na wewe amekupitia?” “Mi napita tu wajamani.”“Mambo ni moto, hana ngoma mzee baba…tehe.”“Kwi, kwiii, kwiiiiiii.” Hizi zilikuwa ni baadhi ya fleva za wachangiaji katika posti hiyo huko kwingineko nako hakukua shwari.

MSURURU WA WAREMBO WATAJWA

Waliokuwa wanaonesha wasiwasi, walikwenda mbali zaidi kwa kuweka mezani warembo ambao wamewahi kuwapitia’ mkali huyo wa Bongo Fleva hususan wale mastaa na kuongeza na wale wasiojulikana.

“Jamani tuwe wakweli, we msururu wa warembo alionao Diamond kweli anaweza kuwa salama?” Alihoji mmoja wa wachangiaji mtandaoni. Mchangiaji mwingine alizidi kushusha data kwa kuanika msururu wa warembo wanaodaiwa kutembea na Diamond na kuanzia na Wema Sepetu (muigizaji), Jokate Mwegelo (modo na muigizaji), Penniel Mungilwa ‘Penny’ (mtangazaji), Irene Uwoya (muigizaji), Hamisa Mobeto (mwanamitindo), Lynn (modo) na Rehema Fabian (miss), orodha hii ibaki kuwa mali ya wachangiaji mitandaoni na siyo ya Amani.

Kuwekwa mezani kwa warembo hao na wengine wakidai hao ni baadhi tu ya watu maarufu na kwamba wapo wengine pia wasiokuwa mastaa, bado wengine waliiponda orodha hiyo kwa kusema haina mashiko kwani suala la Ukimwi linabaki kwenye hoja ya kupata mchubuko kati ya watu wawili wanaposhiriki tendo la ndoa.

DAKTARI ANENA

Ili kupata uelewa mpana wa jambo hilo lililozua gumzo mtandaoni, Ijumaa lilizungumza na daktari maarufu jijini Dar, Dk Chale ambaye alieleza kuwa, maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi husababishwa na mambo mbalimbali. Alisema ngono zembe huchangia, mtu kushea vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi kama sindano na wembe.

Mbali ya hilo, alisema upo uwezekano mdogo wa mtu kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi na asipate maambukizi endapo hakutatokea mchubuko. “Lakini ni kwa asilimia chache sana mtu anaweza asipate mambukizi na ndiyo maana wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya wanashauri kujikinga kwa kuvaa kondomu,” alisema dokta Chale.

MAJIBU YA DIAMOND YAKOJE?

Ijumaa lilimvutia waya juzi Diamond ili kutaka kujua anazungumziaje ishu hiyo na kama atakuwa tayari kuanika majibu ya vipimo vyake lakini simu yake ilikuwa haipatikani. Hata hivyo, mtu wa karibu na Diamond alieleza kuwa kwa wakati huo msanii huyo alikuwa safarini hivyo huenda ndiyo sababu ya kutompata kwa urahisi.

TUJIELIMISHE

Kama jamii suala la unyanyapaa ni la kupingwa na kila mtu, kwani haifai hata kidogo kunyoosheana vidole katika suala la Ukimwi kwani kufanya hivyo kunachangia kulikuza tatizo. Ifahamike pia kwamba mtu kuambukizwa Ukimwi hakutokani na wingi wa wapenzi alionao mtu bali kupuuza kutumia kinga katika kila tendo la ndoa, jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kuwa na umakini nalo ili kulipiga vita gonjwa hilo.

STORI: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi 
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Follow fav football team, live score & comentary

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Ripoti tatizo

159Chukia

COPY SUCCESS

July 30, 2018

DORTMUND WAFIKA BEI KWA SAMATTA

DORTMUND WAFIKA BEI KWA SAMATTA

dimba.co.tz

Jul 29, 2018 2:32 PM

NA SAADA SALIM     |      

NAHODHA wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, amezidi kuziumiza vichwa baadhi ya timu kubwa barani Ulaya baada ya Borussia Dortmund, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu Bundesliga, kuihitaji saini yake.

Tayari Levante inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ imeshaweka mezani Euro milioni 4 ili kuinasa saini ya Mtanzania huyo huku timu yake ya Genk ya Ubelgiji, ikisema kiasi hicho cha fedha ni kidogo kulinganisha na uwezo wa mchezaji wao.

Akizungumza jana na DIMBA jana, Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema Dortmund pamoja na Metz ya Ufaransa nazo zinaitaka huduma ya Samatta japo Levante ndio walioko kwenye kasi kubwa.

“Licha ya kwamba Levante ndio wameenda rasmi lakini hata Borussia (Dortmund) na Metz, nao wameonyesha nia ya kuitaka saini yake, nadhani muda sio mrefu kila kitu kitakuwa wazi,” alisema.
Kama Dortmund watafika bei inamaanisha Samatta atakwenda kugombania namba na akina Shinji Kagawa na Mario Gotze.

Katika hatua nyingine Samatta leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Lokeren, mchezo wao wa ufunguzi Ligi Kuu nchini Ubelgiji.

Msimu mpya wa ligi nchini humo umeanza juzi Ijumaa na Genk ya Samatta, wao wanaianza safari yao ya kuusaka ubingwa leo ugenini dhidi ya wapinzani wao hao Uwanja wa Daknamstadio.

Baada ya mchezo huo wa ligi, kikosi hicho cha Genk kitakuwa na kazi nyingine Jumatano kucheza na Fola Esch mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Europa League.

Genk wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwani mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana katikati ya wiki hii, kikosi hicho cha akina Samatta kilishinda mabao 5-0 nyumbani.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Ripoti tatizo

177Chukia

COPY SUCCESS