ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Monday, July 30, 2018

KCB BANK TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA

KCB BANK TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA
Erasto blog.com

Jul 30, 2018 11:23 AM

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario  na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia wakikabidhiana mkataba baada ya kusaini Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420.000.000  katika hoteli ya Serena leo jijini Dar es salaam kulia ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420.000.000 kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya kusaini  mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCM Bi. Fatma Chilo wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa KCB Bank na TFF.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario akizungumza katika mkutano huo.

Baadhi ya watendaji wa benki ya KCB wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio katika mkutano huo.

………………………………………………………………….

KCB Bank Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa mwaka 2018/2019. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania 420,000,000 ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
KCB Bank Tanzania imeongeza thamani ya udhamini wake kwenda ligi hiyo kutoka kiasi cha shilingi za Kitanzania 325,000,000 msimu wa 2017/18 mpaka shilingi 420,000,000 msimu wa 2018/19 ongezeko la ziadi ya milioni 90,000,000, ongezeko linaloashiria dhamira ya benki hiyo kutaka kunyanyua vipaji na kuendeleza ushindani katika mpira wa miguu nchini Tanzania.
Hafla ya kutia saini makubaliano hayo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi. Fatma Chillo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi KCB Bank Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba mchango wa kiuchumi unaoletwa na soka ni mmoja sababu kubwa zilizopelekea KCB Bank Tanzania kutaka kudhamini ligi hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo. “Tunaamini kuwa sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kwani ni chanzo cha ajira kwa watanzania hasa vijana.” alisema Nd. Kimario.
Kaimu Menyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi. Fatma Chillo alisema kuwa ni fursa ya kipekee kuweza kudhamini Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili. “Lengo letu ni kuleta hamasa kwa timu na mashabiki wa mpira wa miguu kwa kuzijengea timu, hata zile ndogo uwezo wa kifedha ili kuziwezesha kushindana kikamilifu hivyo kuongeza ushindani ndani ya ligi.” Alieleza Bi. Chillo.

Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru KCB Bank Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2018/19. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

155Chukia

COPY SUCCESS

No comments:

Post a Comment