DORTMUND WAFIKA BEI KWA SAMATTA
dimba.co.tz
Jul 29, 2018 2:32 PM
NA SAADA SALIM |
NAHODHA wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, amezidi kuziumiza vichwa baadhi ya timu kubwa barani Ulaya baada ya Borussia Dortmund, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu Bundesliga, kuihitaji saini yake.
Tayari Levante inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ imeshaweka mezani Euro milioni 4 ili kuinasa saini ya Mtanzania huyo huku timu yake ya Genk ya Ubelgiji, ikisema kiasi hicho cha fedha ni kidogo kulinganisha na uwezo wa mchezaji wao.
Akizungumza jana na DIMBA jana, Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema Dortmund pamoja na Metz ya Ufaransa nazo zinaitaka huduma ya Samatta japo Levante ndio walioko kwenye kasi kubwa.
“Licha ya kwamba Levante ndio wameenda rasmi lakini hata Borussia (Dortmund) na Metz, nao wameonyesha nia ya kuitaka saini yake, nadhani muda sio mrefu kila kitu kitakuwa wazi,” alisema.
Kama Dortmund watafika bei inamaanisha Samatta atakwenda kugombania namba na akina Shinji Kagawa na Mario Gotze.
Katika hatua nyingine Samatta leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Lokeren, mchezo wao wa ufunguzi Ligi Kuu nchini Ubelgiji.
Msimu mpya wa ligi nchini humo umeanza juzi Ijumaa na Genk ya Samatta, wao wanaianza safari yao ya kuusaka ubingwa leo ugenini dhidi ya wapinzani wao hao Uwanja wa Daknamstadio.
Baada ya mchezo huo wa ligi, kikosi hicho cha Genk kitakuwa na kazi nyingine Jumatano kucheza na Fola Esch mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Europa League.
Genk wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwani mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana katikati ya wiki hii, kikosi hicho cha akina Samatta kilishinda mabao 5-0 nyumbani.
Tazama yote
Fungua Opera News ili kusoma zaidi
Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.
177Chukia
COPY SUCCESS
Comments
Post a Comment