Yanga yamalizana na vifaa vitatu
globalpublishers.co.tz
Dec 3, 2018 6:19 PM
KAMATI ya Usajili ya Yanga, rasmi imethibitisha kufikia uwezekano wa asilimia 90 kuwasajili wachezaji watatu katika usajili huu wa dirisha dogo.
Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu Yanga imshushe winga wake raia wa DR Congo, Reuben Bomba ambaye yupo nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo kabla ya kumsainisha mkataba wa kukipiga Jangwani.
Timu hiyo, tofauti na kuwa na mazungumzo na Mkongo huyo, zipo tetesi za kumsajili beki wa Lipuli FC, Ally Mtoni ‘Sonso’ na mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile ambaye ni kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatatu,Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alisema kwa asilimia 90 mipango yao ya usajili imekamilika, hivyo wakati wowote watawasajili wachezaji hao.
“Niwatoe hofu mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa mipango yetu ya usajili imekamilika kwa asilimia 90, hivyo kilichobakia ni kumalizana na wachezaji hao aliowahitaji kocha.
“Tayari kocha ameshatukabidhi ripoti yake ya usajili akihitaji winga, beki wa kati, mshambuliaji na kiungo mmoja mkabaji ambao tayari tumewapata, kilichobakia ni kuwasajili pekee.
“Hakuna kitakachoshindikana kwetu, licha ya uchumi wetu kuyumba, matarajio yetu ni kuona timu ikifanya vizuri katika mzunguko wa kwanza baada ya kukamilisha mahitaji ya kocha katika usajili wetu,” alisema Nyika.
Tazama yote
185Chukia
COPY SUCCESS
Comments
Post a Comment