ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Thursday, August 16, 2018

JESHI LA POLISI LATII AGIZO LA KUKAMATA WANAKIJIJI WOTE KIJIJI CHA NGOLE, MBEYA.

JESHI LA POLISI LATII AGIZO LA KUKAMATA WANAKIJIJI WOTE KIJIJI CHA NGOLE, MBEYA.

darmpya.com

Aug 16, 2018 1:59 PM

Tayari magari yaliyosheheni maaskari wa kutosha yametumwa katika Kijiji cha Ngole kilichopo kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwaajili ya kuwakamata wanakijiji hao kutokana na kutuhumiwa kuharibu mradi wa maji katika kijiji jirani cha Msheye.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyepo kijijini hapo amedai kuwepo kwa hofu kubwa miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amenukuliwa na chombo kimoja cha habari nchini, akithibitisha kuwatuma askari wake kwaajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Mapema siku ya jana RC Chalamila aliagiza Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kuwakamata wanakijiji wote wa kijiji cha Ngole kwa tuhuma za kuharibu mradi wa maji katika kijiji cha Msheye, ambapo alikitaja kitendo hicho kuwa ni uhujumi uchumi na hivyo wanakijiji hao lazima washughulikiwe ipasavyo.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

20Chukia

COPY SUCCESS

No comments:

Post a Comment