ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Monday, July 9, 2018

yajue mambo ya msingi yanayofaa kuwa katika chumba chako

Vitu vinne usivyotakiwa kuvikosa chumbani

mwananchi.co.tz

Jul 9 2018 3:00 PM

Kila mtu ana mapenzi yake katika maisha lakini kuna baadhi ya vitu hufanana na hata vikipishana ni kidogo kulingana na mazingira. Leo nimekuletea vitu vitano ambavyo kila mmoja anapaswa kuwa navyo chumbani kwake bila kujali anaishi wapi na katika hali gani.

Zulia

Zulia ni muhimu kuwa nalo chumbani. Kuna wanaopenda la manyoa au la kawaida na wapo pia wanaopenda lililojaa chumba kizima au nusu, hiyo yote ni juu ya muhusika. Cha kuzingatia hakikisha humwagii vitu vyenye majimaji kwa sababu likiingia maji litanuka na kuwa kero ndani.

Mtindo wa samani za chumbani (theme)

Wengi hudhani hii itapendeza chumba cha watoto. La hasha hata chumba cha makubwa inastahili. Unaweza ukaaamua rangi gani itamalaki ndani mwako iwe ya kupoa au kung’aa cha msingi ni kuwa na theme ya chumba hii inakifanya kiongeze mvuto.

Chumba hasa kitandani kunapaswa kuwa na mito ya aina mbalimbali ikiwamo ya kulalia na mapambo.

Itapendeza zaidi ikiwapo mipana na mirefu, maarufu mito ya pipi.

Ni vyema na itapendeza chumbani kukiwa na eneo la kukaa mbali ya kitandani. Eneo hilo unaweza kuweka kochi au kiti kipana kitakachokupa faraja ukikikalia.

Siyo vibaya kujiweka picha chache za familia na za ukutani. Hakikisha picha za ukutani siyo za watu wala zinazotisha, unaweza kuweka zenye mandhari ya bahari, uoto wa asili na nyinginezo.

Kama una tuzo ulizowahi kuipata, basi ndiyo mahali pake na kwa ajili ya kuhifadhi vitu vya aina hii ni muhimu kuwa na droo kubwa kiasi pembeni ya chumba kwa ajili ya vitu hivyo

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Follow fav football team, live score & comentary

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Ripoti tatizo

197Chukia0762995785

COPY SUCCESS

No comments:

Post a Comment