ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Friday, July 27, 2018

PAZIA LA USAJILI; YANGA WAFANYA MAAJABU DAKIKA ZA MWISHO, SIMBA YAMBAKIZA NDEMLA -

Kipa Klaus Nkinzi Kindoki kutoka DRC (kulia) akikabidhiwa jezi na Meneja w aYanga, Hafidh Saleh 

Geoffrey Mwashiuya akifurajia na jei ya Singida Unioted baada ya kusiani mkataba w miaka miwili kutoka Yanga SC

Yanga SC imefanikiwa kumbakiza beki wake tegemeo, mkongwe Kelvin Yondan, lakini imenasa saini za wachezaji wawili kutoka  kipa Klaus Nkinzi Kindoki na mshambuliaji Heritier Makambo, ambaop kila mmoja kusaini mkataba wa miaka miwili.
Wachezaji hao walikuwa kwenye majaribio Yanga kwa wiki kadhaa chini ya kocha Mwinyi Zahera wa Yanga SC, Mkongo mwenzao pia.
Lakini pia Yanga imempoteza beki wake wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy aliyehamia Nkana FC ya Zambia, huku jaribio la kuwapeleka kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake, akiwemo kipa Youthe Rostand likikwama dakika za mwishoni. 
Azam FC imemsajili mshambuliaji Daniel Lyanga kutoka Singida United alikocheza kwa muda mfupi tu akitokea Fanja SC ya Oman, ambayo ilimnunua Simba SC mwaka juzi.
Singida imeziba pengo la Lyanga kwa kuwasajili winga Geoffrey Mwashiuya kutoka Yanga na mshambuliaji Mghana, Hans Kwofie akitokea Smouha S.C ya Misri kila mmoja akisaini mkataba wa miaka miwili.


Beki na Nahodha, Kevin Yondan akisaini mkataba wa kubaki Yanga jana

Hadi Alhamisi jioni, TFF ilisema ni klabu moja tu, African Lyon ilikuwa haijakamilisha usajili, lakini Bin Zubeiry Sports – Online imezungumza na Rais wa klabu hiyo, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ ambaye amesema kwamba wamekamilisha usajili wao ndani ya muda.
“Usajili una muda wake maalum wa mwisho, na sisi tuliuzingatia kuhakikisha tunasajili kulingana na taratibu. Tunashukuru, suala la usajili kwetu limepita na limekwenda vizuri,”alisema, Zamunda.   
TFF inatarajiwa kutoa ripoti kamili Ijumaa mchana juu ya namna zoezi lilivyokwenda hadi kukamilika kwake.

Tazama yote

Fungua Opera News 

No comments:

Post a Comment