ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Sunday, July 29, 2018

Jokate Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuteuliwa na Rais Kuwa Mkuu wa Wilaya

Jokate Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuteuliwa na Rais Kuwa Mkuu wa Wilaya

udakuspecially.com

Jul 29, 2018 11:28 AM

From Jokate - Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu.

Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi. Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako. Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu. .

Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi 
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

138Chukia

COPY SUCCESS

No comments:

Post a Comment