ERASTO BLOG

MICHEZO NA BURUDANI

Recent Posts

LightBlog

Breaking

Sunday, July 22, 2018

Beki wa yanga kelvin yondan achana mkataba mnono simba!

Call 0718041230

BEKI wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, ameweka wazi kuwa, alitengewa donge nono la Sh milioni 100 na Simba ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini akakataa kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo na Wanajangwani hao.

Akizungumza na DIMBA jana, Yondani alikiri kukutana na vigogo wa Simba Jumanne ya wiki hii na kuzungumza nao, huku akiwekewa mezani kitita hicho cha fedha, lakini baada ya kutafakari kwa kirefu akaona ni bora abakie Yanga ili kulipa fadhila.

ìKweli jamaa Simba nilizungumza nao wakataka kunipa milioni 100 na mkataba wa miaka miwili, lakini baada ya kufikiria sana nikakataa, kwani naiheshimu sana Yanga na ningependa nimalize soka langu katika klabu hiyo.

ìLicha ya kwamba Yanga haikufika dau hilo la Simba, lakini niliona nisaini, kwani nilishajiwekea mwenyewe kwamba ninataka kumalizia soka langu hapo, nathamini mchango wao kutokana na jinsi nilivyoishi nao vizuri katika shida na raha,î alisema.

Licha ya kwamba Yondani hakutaka kuweka wazi dau alilotengewa mezani na Yanga, lakini DIMBA limepenyezewa taarifa kuwa, milioni 60 ndizo alizopewa, huku akikacha milioni 100 za Simba.

Jumanne ya wiki hii ndiyo zilivuja taarifa za Simba kufanya mazungumzo na Yondani na kama beki huyo asingekuwa na mapenzi ya dhati na Yanga, bila shaka angesaini, kwani fedha aliyotengewa ilikuwa kubwa.

Akizungumza na DIMBA jana, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuiokoa Yanga katika kipindi hiki kigumu, Abas Tarimba, alisema kwa sasa mashabiki wa Klabu hiyo wasiwe na wasiwasi wowote juu ya beki huyo, kwani wameshamaliza kazi.

Nimefanya hivyo kumrudisha kundini Yondani kama mwanachama na mkereketwa wa Yanga, mashabiki sasa wasiwe na wasiwasi, kwani beki huyo msimu ujao ataichezea timu yetu,î alisema.

Alipoulizwa kuhusu zoezi zima la usajili wakati huu ambao hatua hiyo imekuja zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha, alisema kuhusu usajili wa wachezaji wengine yeye hajui lolote na kwamba wenye jukumu hilo ni viongozi waliopo madarakani.

Dimba lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Yanga, Hussein Nyika, kutaka kujua endapo baada ya Yondani kuna usajili wa wachezaji wengine unaoendelea, lakini alikataa kuzungumzia suala hilo, akisema kwamba yeye ni mgonjwa na yupo kitandani.

“Siwezi kuzungumzia suala hilo hivi sasa nipo kitandani ninaumwa,” alisema.

Pia Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam ambaye hivi karibuni aliongoza kikao cha wanachama kwa ajili kujua hatima ya maendeleo ya usajili na mambo mengine yanayohusu maendeleo ya klabu hiyo, alisema naye hawezi kuzungumzia kwa vile jana alikuwa katika sherehe za CCM.

Tazama yote

Fungua Opera News ili kusoma zaidi

Offline reading without Internet. Download 1000+ news in just 10 seconds.

Follow fav football team, live score & comentary

Ripoti tatizo

147Chukia

COPY SUCCESS

No comments:

Post a Comment